ZIARA YA BODI YA TRL VITUO VYA KIGOMA, MPANDA NA MWANZA..JULAI 14-18, 2017

kigoma 258

kigoma 46

kigoma 50

kigoma 76

kigoma 81

kigoma 89

kigoma 106

kigoma 115

kigoma 121

kigoma 128

kigoma 156

kigoma 161

kigoma 163

kigoma 165

kigoma 174

kigoma 186

kigoma 188

kigoma 193

kigoma 195

kigoma 223

kigoma 232

kigoma 236

kigoma 237

kigoma 240

kigoma 244

kigoma 155BODI YA TRL YATEMBELEA VITUO VYA KIGOMA, MPANDA NA MWANZA ( JULAI 14-18, 2017)

na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Bodi ya TRL Profesa John Wajanga Kondoro amewataka Wanareli kote aliposimama kuzungumza nao kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu kutatua zile changamoto zilizo ndani ya uwezo wa mamlaka za Wilaya za Reli.
” Kusubiri hadi Bodi na Mkurugenzi Mtendaji kumweleza changamoto za kawaida ni sawa na kukiri kuwa Maafisa Waandamizi wa Wilaya TRL wameshindwa majukumu yao” Alisisitiza Mwenyekiti. Akawataka kujiongeza, mathalani kwa kazi ya kutunza mazingira na kuweka usafi wa maeneo ya reli kupanua huduma za vyoo nakadhalika .

Alisema ni kwa zile changamoto zinazohitaji maamuzi ya Makao Makuu na fedha nyingi ndio za kuelekezwa Makao Makuu. Aliwashauri hata kwa changamoto kubwa zinapaswa kujadiliwa katika ngazi za Wilaya , Idara na ikishindikana inapelekwa kwa Mkurugenzi Mkuua hadi ngazi ya Bodi.

Alisema kwa jinsi Serikali ilivyoweza kuwekeza kwa kutupa vitendea kazi tunapaswa kuwa tayari kujibu swali la mwekezaji Mkuu Serikali siku itakapowauliza Wanareli kwa huu mtaji wa vitendea kazi hivi vya zaidi ya bilioni 250, hivi mmevitumiaje na mmezalisha kiasi gani. ” Kama hatutakuwa na jibu Serikali itaona sote hapa hatufai bora itafute mbadala wetu.
Hata hivyo kihistoria Wanareli ni moja ya Kada iliyo imara sana na ndio maana hadi sasa reli ya kati bado ipo. “ Changamoto ya jumla ni kuweza kuimarisha miundo mbinu na kuwezesha kuwapa imani Wadau wetu ili mizigo yote iliohamia barabarani irejee relini. Aidha tuwe na uwezo wa kubuni mazingira ya gharama ambayo reli itakuwa ina unafuu wakati huohuo kuhakikisha inapata mapato ya kutosha ili siku moja tuiambiye Serikali msaada wake wa kutupatia mshahara basi. Pia Mwenyekti alisisitiza ulazima wa kuopiga vita hujuma zote kuanzia wizi wa mafuta na shehena za Wateja.
Alifafanua baadhi ya wateja huiweka Menejimenti katika mazingira magumu kwa kuwauiliza bila ya kumeza mate kuwa ‘mnataka tusafirshe shene zetu katika reli je tabia yenu ya wizi mmeiwacha?’.

Mwenyekiti ametoa wito kwa kuanzia Wanareli binafsi hadi kupitia viongozi wa Chama chao TRAWU na Menejimenti kufanya kazi kwa ushirikiano wa kitimu. ‘ Wote tunatakiwa tupeleke nguvu zetu uopande mmoja moja”. Mwenyekiti alisisitiza. .
Aidha Mkurugenze Mtendaji Nd Masanja Kadogosa ameelezea jitihada za uongozi wake kutatua kero zikiwemo malimbikizo ya makato katika Bima ya Afya NHIF, Wadu, NSSF kuwa katika kipindi kifupi zaidi ya Shilingi bilioni 6 za malimbikizo zimelipwa. Na kwamba Mkakati umewekwa kumaliza madeni hayo katika muda mfupi uwezekanavyo kulingana na uzalishaji wa kampuni. Katika ziara hiyo Mwenyekiti Prof Kondoro alifuatana na Wajumbe wote wa Bodi wakiwemo Mama Martha maeda, Mama Mariam Mwanilwa. Wengine ni Mzee Linford Mboma, Mhandisi Cherles Mvungi, Mhandisi Karim mattaka na Mkurugenzi Mahamud Mabuyu. Aidha ziara hiyo walikuwepo Maafisa waandamizi wa TRL kadhaa.
Ziara hiyo ilianza Julai 14, 2017 Kigoma na kumalizika Mwanza Julai 18, 2017. Baadhi ya maeneo yalitembelewa na Bodi ni pamoja na Kigoma mjini, ikiwemo  ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bandari ya Kigoma na Stesheni ya Reli ya Kigoma. Aidha pia Bodi ilitembelea Mpanda Stesheni za  Katumba , Isaka, Shinyanga, Malya.
Jijini Mwanza Bodi ilipata fursa ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela. Baadae ujumbe ukatembelea bandari ya Mwanza Kaskazini na pia Mwanza Kusini na  kuhitimisha kwa kuzungumza na Wanareli wa Mwanza katika eneo la karakana. Ujumbe huo wa Bodi ulirejea Dar es salaam jioni Julai 18, 2017.

Leave a Reply