HUDUMA YA TRENI ZA ABIRIA NA MIZIGO KUHAMISHIWA MOROGORO KUANZIA KESHO!

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)

 

     

 

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI –PRESS RELEASE

 SAM_0537

HUDUMA YA TRENI ZA ABIRIA NA MIZIGO  KUANZIA MOROGORO HAPO KESHO JUMAMOSI MEI 20, 2017

 

Uongozi  Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kuhamishia kwa muda huduma ya usafiri wa treni kwenda bara katika kituo cha Morogoro kuanzia kesho Jumamosi Mei 20, 2017, badala ya  Dar es Salaam. Abiria watakaohusika ni wale wenye tiketi waliokuwa waondoke leo  Ijumaa na wale wa Jumapili ambao treni zao zimefutwa.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya TRL abiria wanatakiwa wafike kituo kikuu cha Reli Dar es Salaam kesho Jumamosi  kabla ya .saa  Moja asubuhi ambapo watasafirishwa kwa mabasi maalum yaliyokodiwa na TRL hadi Morogoro ambako watapanda  treni kwenda bara itakayoondoka  saa Moja kamili usiku.

 

Kuhusu Wafanya biashara  wasafirishaji wa shehena kwenda bara wametakiwa kuwasiliana na Idara ya masoko ya TRL ili kupewa utaratibu wa jinsi ya kusafirisha mizigo yao hadi Morogoro ambako itasafirishwa kwa treni kwenda bara.

Uamuzi huu umechukuliwa kufuatia kipande cha reli kati ya Dar es Salaam na Ruvu kuwa hakipitiki baada ya daraja la reli la Ruvu kutitia upande mmoja

 

Mamlaka husika zinafanyia kazi ukarabati wa daraja hilo ili njia ya reli kutoka hadi Morogoro  ifunguliwa kwa muda mfupi iwezekanavyo.

 

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya TRL Profesa John Kondoro na wajumbe wengine wa Bodi asubuhi hii wametembelea eneo la daraja ambapo walifanya tathmini na  Bodi kama mamlaka ilitoa  maelekezo yake kwa Menejimenti ya TRLi  kuhusu maandalizi  na utekelezaji wa  kazi za ukarabati wa daraja hilo..

 

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:

Kwa Niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KampunI ya Reli Tanzania(TRL),

Ndugu Focus Makoye Sahani,

Mei 19, 2017

DAR ES SALAAM

SAFARI ZA TRENI KWENDA BARA ZASITISHWA KUANZIA LEO MEI 18, 2017

 

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)

 

     

 

                                                                 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI –PRESS RELEASE

 

KUSIMAMISHWA HUDUMA YA TRENI ZA ABIRIA KWENDA BARA KUANZIA LEO MEI 18, 2017

 

Uongozi  Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusimamishwa huduma ya treni za abiria kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuanzia leo Mei 18, 2017 hadi itakapotangazwa tena.

 

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kutokea uharibifu wa miundombinu ya reli leo asubuhi kati ya stesheni za Ruvu na Ruvu junction uliosababishwa na mvua kubwa zinazonyeshwa maeneo hayo ya mkoa wa Pwani.

 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo  ya kusitisha huduma kwa muda treni ya abiria ya deluxe iliokuwa iondoke Dar es Salaam leo saa 2 asubuhi imefutwa na abiria wametakliwa wafike stesheni ili warejeshewe fedha zao za nauli.

 

Wakati huo huo Uongozi wa TRL tayari umeelekea eneo la tukio ili kufanya tathmini na kupanga mikakati ya haraka kukarabati miundo mbinu husika likiwemo daraja la Ruvu.

 

Aidha Uongozi umefafanua katika taarifa yake kuwa katika kipindi cha mpito, treni ya abiria kutoka Kigoma na Mwanza kuja Dar es Salaam itaishia Morogoro hadi njia ya reli  kati ya Dar es Salaam na Morogoro  itakapofunguliwa tena.

 

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:

KampunI ya Reli Tanzania(TRL),

Mei 18, 2017

DAR ES SALAAM 

Treni ya Deluxe picha ya maktaba TRL
Treni ya abiria ya  Deluxe ikiwa Stesheni ya Morogoro picha ya maktaba TRL

UONGOZI WA TRL WAMEZINDUA HUDUMA  MAALUM YA USAFIRISHAJI SHEHENA WA ‘BLOCK TRAIN KWENDA BURUNDI MACHI 31, 2017 KUTOKA MALINDI YARD BANDARINI.

burundi block train 1
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  wa TRLNd Shaban Kiko akipunga bendera kuashiria kuazna safari ya ‘block trani’ yenye mzigo wa mteja wetu UBUCOM kutoka Burundi hapo Machi 31, 2017 Malindi Yard bandarini Dar es Salaam.

 

 

Imefahamika kuwa  huduma maalum ya usafirishaji shehena wa treni nzima ‘block train’ imezinduliwa rasmi na Uongozi  wa TRL kwenda Burundi katika  kituo cha Malindi bandarini Dar es Salaam Machi 31, 2017.

 

Huduma ya block train iliozinduliwa ni maalum kwa wafanyabiashara na kampuni binafsi  wenye  shehena  kubwa za mizigo kutosheleza mabehewa 20 ambapo hurahisisha kuisafirisha moja kwa moja hadi kwa mpokeaji( mwenye mzigo).

 

Kwa mujibu wa taarifa ya Uongozi wa TRL treni hiyo yenye mabehewa 20 imebeba malighafi ya chuma( iron coils) mzigo unaosafirishwa na Kampuni ya UBUCOM ya Burundi na utachukua muda wa siku 3 kuwasili Kigoma na siku moja kuwasili mjini Bujumbura. Burundi.

 

Aidha taarifa zaidi zimeainisha kuwa TRL imepunguza gharama za usafirishaji wa mizigo ya kawaida (loose cargo) na ile iliohifadhiwa katika makasha kwenda Burundi. Hivi sasa TRL inatoza jumla ya Dola za Kimarekani (USD)3,056 kwa behewa moja la mizigo ya kawaida na USD 3024/= kwa mizigo iliofungwa katika makasha hadi Bujumbura Burundi ikilinganishwa na  gharama ya  USD 3500/= ikisafirishwa barabarani.

Gharama za TRL zinahusisha pia  uhudumiaji shehena bandarini  Dar es Salaam, Kigoma na Bujumbura na pia usafiri wa reli hadi Kigoma na wa meli hadi Bujumbura.

burundi block train
Mandhari ya Kituo cha Malindi wakati ‘block train’ ya Burundi ikijitayarisha kuondoka Ijuumaa Machi 31, 2017

 

 

HUDUMA YA TRENI YA PUGU AWAMU ZOTE KUWA NA SAFARI 3 KUANZIA MACHI 27, 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
 
 
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) unawatangazia watumiaji wa huduma ya treni ya Jiji iendayo Pugu kuwa kuanzia Jumatatu Machi 27, 2017 ratiba yake ya kawaida ya safari 3 kwa awamu ya asubuhi na alasiri itaanza tena.
 
Taarifa imeainisha kuwa kazi ya kutandika reli nzito ratili 80 imekamilika kwa asilimia 75 tokea ilipoanza pale Januari 03, mwaka huu wa 2017. Kati ya vituo vya reli vya Dar es salaam na Pugu ni kuna umbali wa kilomita 20.
 
Safari ya treni kutoka kituo cha Pugu kwenda kituo Kikuu cha Dar es Salaam kwa awamu ya asubuhi ya kwanza itaondoka saa 12 asubuhi juu ya alama ya pili saa 2:10 na ya tatu saa 4:20.
Aidha jioni treni ya kwanza itaondoka Kituo Kikuu cha Dar kwenda Pugu saa 9::55 alasiri, ya pili saa 12:05 magharibi na ya tatu ambayo ni ya mwisho itaondoka saa 2:15 usiku. Atakayesoma taarifa hii amuarifu na mqwenzake.
 
Uongozi wa TRL unawashukuru sana wateja wake wa Pugu kwa kwa ushirkiano walioutoa katika kipindi chote cha uakarabati wa reli kati ya Kituo Kikuu cha Dar es Salaam na cha Pugu.
 
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Nd. Masanja Kadogosa,
Dar es Salaam,
Machi 25, 2017.1909700_10209313935753670_1272537156472894348_n

SALAAM ZA MWAKA MPYA WA 2017 KWA WANARELI KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL ND. MASANJA KUNGU KADOGOSA

SALAAM ZA MWAKA MPYA WA 2017 KWA WANARELI KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL

ND. MASANJA KUNGU KADOGOSA

 

 

Nd Masanja Kadogosa


Ndugu Wanareli Wenzangu;

Nawatakia Mwaka mpya 2017 mwema, kama nilivyotangulia kusema awali, Naamini 2017 utakuwa wa mafanikio makubwa kwenye sekta ndogo hii ya Reli, kila mmoja wetu atimize wajibu hapo alipo, kabla ya kunyoshea kidole mwenzako, jiulize kwanza uwepo wako na unachokifanya kinaharakisha kuyafikia yale 

Wanarelii wote tumedhamiria. Tumefanya mengi 2016, tunakila sababu ya kujipongeza na kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi Rehema. Hata hivyo ni vyema tukafahamu adui wa kwanza katika uongozi ni yale mafanikio ya mwisho, ni rahisi uongozi kujisahau na kuzani kila jambo linaenda vyema, mwaka 2017 tutazikabili changamoto zetu kwa nguvu zote, dhamira ya uongozi ni kuona wafanyakazi wetu wanaishi kama wafanyakazi wengine kwenye taasisi za serikali. Kwa pamoja haya yote yanawezekana.

Wasalaam ,

MASANJA KUNGU KADOGOSA

MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL

TRENI YA ABIRIA YA KESHO JUMANNE YAAHIRISHWA HADI KESHOKUTWA JUMATANO!

posted in: Emergency Notices | 0

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)

TRENI YA ABIRIA YA KESHO JUMANNE KUONDOKA JUMATANO SEPTEMBA 14, 2016 SAA TISA ALASIRI

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusogeza mbele kwa siku moja safari ya treni ya abiria ya Jumanne kwenda bara kutoka Dar es Salaam. Treni hiyo itaondoka Jumatano Septemba 14, 2016 saa 9 alasiri.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kusogezwa mbele ni kutokana na kipande cha treni kutoka Kigoma kuchelewa kufika Tabora. Treni hiyo wakati ikienda Kigoma ilicheleweshwa kufika Kigoma baada ya treni ya mizigo kupata ajali kati ya stesheni za Kazuramimba na Luiche..

Uongozi wa TRL unawaomba radhi abiria na wananchi kwa ujumla kwa usumbufu utakaojitokeza
Atakayesoma taarifa hii amwarifu mwenzake.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
1909700_10209313935753670_1272537156472894348_nNdugu Masanja Kungu Kadogosa
Dar es Salaam,
Septemba 12, 2016

TRENI YA 3 YA ABIRIA YA KAWAIDA KUANZA JUMAPILI SEPTEMBA 04, 2016

SAM_0536KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)

(TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)
TRL YAFANYA MABADILIKO YA RATIBA YA SAFARI ZA ABIRIA KWENDA BARA NA KUONGEZA MOJA KUANZIA SEPTEMBA 01 , 2016

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umeamua kuongeza safari ya tatu ya treni ya abiria ya kawaida kwenda bara ambayo itaondoka Dar es Salaam kila Jumapili, safari ya kwanza itakuwa Jumapili hii ya Septemba 04, 2016 saa 9 alasiri.

Taarifa imeainisha kuwa treni hiyo ya huduma ya kawaida itakuwa na mabehewa 12 kutokea Dar es Salaam ikiwa na mabehewa manane ya daraja la 3, mawili daraja la pili kulala na mawili daraja la kwanza. Katika stesheni za Morogoro na Dodoma yataongezwa mabehewa mawili mawili ya daraja la 3.
Aidha treni ya Deluxe imebadilishwa siku ya kuondoka badala ya Jumapili kwa sasa kuanzia Septemba Mosi, 2016 itakuwa inaondoka siku ya Alhamis saa 2 asubuhi kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam.

Halikadhalika mabadiliko haya pia yataongeza safari za treni ya kwenda Mpanda kutoka Tabora badala ya 2 za sasa zitakuwa 3 kwa wiki ambazo ni Jumatatu, Jumatano na Jumamosi..
Wakati huohuo Uongozi wa TRL umefanya uamuzi wa kihistoria wa kupeleka huduma za kuuzwa tiketi za safari zake mjini Kasulu ambapo kuanzia Septemba Mosi itafungua kituo cha Reli ambacho kitafanya kazi ya kuto huduma hiyo kwa wasafari wanaotoka Kasulu mjini na maeneo ya jirani . Kwa uamuzi huo TRL imetoa nafasi za tiketi za behewa moja la daraja la 3. Mpango pia uko mbioni wa kufungua kituo kama hicho siku zijazo mjini Kibondo hali itakaporuhusu kulingana na mahitaji halisi ya abiria.

Taarifa imesisitiza kuwataka wasafiri na wananchi kwa jumla nchini hususan wale wa Mpanda na Kibondo kutumia fursa ya kuongezewa safari na huduma kuletewa karibu kwa kufuata sheria , taratibu na kanuni ili hatua iliyochukuliwa na TRL iwe na tija iliokusudiwa.
Aidha taarifa zaidi zinaarifu kuwa hatimaye TRL imefanikiwa kuongeza mabehewa mawili zaidi ya treni ya Pugu na kufikia idadi ya behewa 18 hadi jana Agosti 22, 2016. Ni matarajio ya Uongozi ifikapo Agosti 31, 2016 treni hiyo ya Jiji itakuwa na mabehewa 20 iloahidi ili kupunguza msongamano unaosababishwa na abiria kuwa wengi katika safari mbili za awali katika awamu zote 2 ya asubuhi na ya jioni.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Focus Makoye Sahani,
Dar es Salaam,
Agosti 23, 2016.1909700_10209313935753670_1272537156472894348_n

ABIRIA YA BARA KUONDOKA SAA 9 ALASIRI NA TRENI YA PUGU KUANZA AGOSTI MOSI!

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)

 

     

 

 

(TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)

KUBADILISHWA MUDA WA KUONDOKA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA KUANZIA AGOSTI  02 ,  2016!

 

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) unatangazwa kubadilishwa muda wa kuondoka treni ya abiria kutoka Dar es Salaaam kwenda bara kuanzia Agosti 02, 2016, ambapo treni  itaondoka saa 9 alasiri ri badala ya saa 11 jioni iliozoeleka. Kutokana na mabadiliko hayo abiria wanatakiwa kufika kituo Kikuu cha reli Dar es Salaam mapema saa 7 mchana.

 

Mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa treni ya pili ya huduma ya Jiji kutoka kituo kikuu  cha reli cha  Dar es Salaam kwenda Pugu ambayo itaanza kutoa huduma Jumatatu Agosti Mosi, 2016.

 

Aidha taarifa ya Menejimenti imefafanua kuwa  mabadiliko hayo yanahusu treni za abiria za huduma ya kawaida zinaondoka siku za Jumanne na Ijumaa. Hata hivyo huduma ya treni ya deluxe itaondoka muda wake wa kawaida kila Jumapili kwenda Kigoma saa 2 asubuhi.

 

Kuhusu huduma ya pili ya treni ya Jiji kwenda Pugu taarifa imefafanua kuwa huduma hiyo itakuwa na vituo 10 vifuatavyo: Pugu Stesheni,  Mwisho wa lami, Gongo la mboto, FFU Mombasa, Banana( njia panda kwenda Segerea), na Karakata. Vingine ni pamoja na Vingunguti Mbuzi, SS Bakhressa, Kamata na Kituo kikuu cha reli Dar es Salaam.

 

Huduma ya treni hiyo itakuwa ya awamu mbili asubuhi na Alasiri ambapo treni ya kwanza itaondoka kituo cha Pugu saa 12 asubuhi na kuwasili kituo cha Dar es Salaam saa 12:55 asubuhi na kufanya safari 3 zitakazomalizika saa 05:15 asubuhi. Jioni pia kutakuwa na safari 3  ambapo treni ya kwanza  itaondoka kituo cha Dar es Salaam saa 09:55 alasiri kwenda Pugu  na kuwasili saa 10:50 jioni na safari ya mwisho kutoka Pugu kuja Dar itakuwa saa 03:20 usiku.

 

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :

Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,

Nd Masanja Kungu Kadogosa,

Dar es Salaam,

Julai 29, 2016.1909700_10209313935753670_1272537156472894348_n1909700_10209313935753670_1272537156472894348_n

1 2