WATATU WAFARIKI KATIKA AJALI YA TRENI NA BASI MOROGORO !

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI( PRESS RELEASE)
 
WATU WATATU WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA TRENI NA BASI MJINi MOROGORO!
 
Watu watatu wamefariki dunia jana saa 12:55 asubuhi katika ajali iliyohusisha basi dogo aina ya Nissan Civilian ilipo gonga treni katika makutano ya Tanesco Morogoro T438 ABR. Mmoja katika hao alifariki katika eneo la ajali ni mwanafunzi anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 6 ambaye bado hajatambuliwa wakati taarifa hii ikichapishwa.
 
Wengine wawili walipoteza maisha wakati wakipelekwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro pamoja na majeruhi wengine 29. Marehemu wametambuliwa kuwa Asha Rashid Mtaalam(16) mwanafunzi wa Kidato cha 3 Sekondari ya Mji Mpya mkazi wa Kigurunyembe na mwingine Rajabu Rashid Kimanga(19) mwanafunzi wa Kidato cha 4 Sekondari ya Tushikamane..
 
Aidha imefahamika majeruhi 29 waliolazwa katika hospitali ya mkoa baadhi yao hali zao sio nzuri.
 
Dereva wa basi aliyesababisha ajali kwa kukaidi kutii amri ya kusimama kutoka kwa Watoa Ishara wa Kampuni ya Reli Tanzania amefahamika kuwa ni Charles Daimon (39) mkazi wa wa Kionda Maghorofani . Polisi wa Kikosi cha Reli wanafuatilia tukio hilo kwa lengo la kumfikisha mahakamani mtuhumiwa.
 
Wakati huo huo Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania umetuma Salaam za rambirambi kwa wafiwa wote waliopoteza watoto wao wapenzi katika ajali hiyo mbaya ya leo asubuhi.
Aidha wamewapa pole majeruhi wote 29 na kuwaombea wapate afueni ya haraka ili warejee katika shughuli zao za kujenga Taifa.Katika kuchangia gharama za mazishi TRL imetoa jumla ya Rambi TZS 2,000,000/= ambapo kila familia ya wafiwa watatu itapewa kila moja TZS Laki Tano na Laki Tano iliyobaki itasaidia gharama za matibabu kwa majeruhi wapatao 33 waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Jumla ya rambirambi hiyo itakabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe Regina Chonjo.ambaye ataratibu ugawaji wake kwa walengwa
 
Halikadhalika TRL imetoa wito kwa watumiaji wa barabara na hasa madereva kufuata na kutii sheria za barabarani ikiwa pamoja kuwa waangalifu wanapofikia makutano ya reli na barabara ili kuepuka maafa na uharibifu wa rasilimali chache tulizo nazo.
 
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano ya TRL kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL ,
Ndugu Masanja Kadogosa,
Dar es Salaam,
Agosti 25, 2017 – Updated

Mhe Regina Chonjo DC wa Morogoro akipokea rambirambi za TRL TZS 2.000,000/= kutoka kwa Mhandisi Adolphina Ndyetabula.hii karibuni
Mhe Regina Chonjo DC wa Morogoro akipokea rambirambi za TRL TZS 2.000,000/= kutoka kwa Mhandisi Adolphina Ndyetabula.hii karibuni

trl ajali moro 3 WATATU WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA TRENI BASI MOROGORO! trl ajali moro 2

ZIARA YA BODI YA TRL VITUO VYA KIGOMA, MPANDA NA MWANZA..JULAI 14-18, 2017

kigoma 258

kigoma 46

kigoma 50

kigoma 76

kigoma 81

kigoma 89

kigoma 106

kigoma 115

kigoma 121

kigoma 128

kigoma 156

kigoma 161

kigoma 163

kigoma 165

kigoma 174

kigoma 186

kigoma 188

kigoma 193

kigoma 195

kigoma 223

kigoma 232

kigoma 236

kigoma 237

kigoma 240

kigoma 244

kigoma 155BODI YA TRL YATEMBELEA VITUO VYA KIGOMA, MPANDA NA MWANZA ( JULAI 14-18, 2017)

na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Bodi ya TRL Profesa John Wajanga Kondoro amewataka Wanareli kote aliposimama kuzungumza nao kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu kutatua zile changamoto zilizo ndani ya uwezo wa mamlaka za Wilaya za Reli.
” Kusubiri hadi Bodi na Mkurugenzi Mtendaji kumweleza changamoto za kawaida ni sawa na kukiri kuwa Maafisa Waandamizi wa Wilaya TRL wameshindwa majukumu yao” Alisisitiza Mwenyekiti. Akawataka kujiongeza, mathalani kwa kazi ya kutunza mazingira na kuweka usafi wa maeneo ya reli kupanua huduma za vyoo nakadhalika .

Alisema ni kwa zile changamoto zinazohitaji maamuzi ya Makao Makuu na fedha nyingi ndio za kuelekezwa Makao Makuu. Aliwashauri hata kwa changamoto kubwa zinapaswa kujadiliwa katika ngazi za Wilaya , Idara na ikishindikana inapelekwa kwa Mkurugenzi Mkuua hadi ngazi ya Bodi.

Alisema kwa jinsi Serikali ilivyoweza kuwekeza kwa kutupa vitendea kazi tunapaswa kuwa tayari kujibu swali la mwekezaji Mkuu Serikali siku itakapowauliza Wanareli kwa huu mtaji wa vitendea kazi hivi vya zaidi ya bilioni 250, hivi mmevitumiaje na mmezalisha kiasi gani. ” Kama hatutakuwa na jibu Serikali itaona sote hapa hatufai bora itafute mbadala wetu.
Hata hivyo kihistoria Wanareli ni moja ya Kada iliyo imara sana na ndio maana hadi sasa reli ya kati bado ipo. “ Changamoto ya jumla ni kuweza kuimarisha miundo mbinu na kuwezesha kuwapa imani Wadau wetu ili mizigo yote iliohamia barabarani irejee relini. Aidha tuwe na uwezo wa kubuni mazingira ya gharama ambayo reli itakuwa ina unafuu wakati huohuo kuhakikisha inapata mapato ya kutosha ili siku moja tuiambiye Serikali msaada wake wa kutupatia mshahara basi. Pia Mwenyekti alisisitiza ulazima wa kuopiga vita hujuma zote kuanzia wizi wa mafuta na shehena za Wateja.
Alifafanua baadhi ya wateja huiweka Menejimenti katika mazingira magumu kwa kuwauiliza bila ya kumeza mate kuwa ‘mnataka tusafirshe shene zetu katika reli je tabia yenu ya wizi mmeiwacha?’.

Mwenyekiti ametoa wito kwa kuanzia Wanareli binafsi hadi kupitia viongozi wa Chama chao TRAWU na Menejimenti kufanya kazi kwa ushirikiano wa kitimu. ‘ Wote tunatakiwa tupeleke nguvu zetu uopande mmoja moja”. Mwenyekiti alisisitiza. .
Aidha Mkurugenze Mtendaji Nd Masanja Kadogosa ameelezea jitihada za uongozi wake kutatua kero zikiwemo malimbikizo ya makato katika Bima ya Afya NHIF, Wadu, NSSF kuwa katika kipindi kifupi zaidi ya Shilingi bilioni 6 za malimbikizo zimelipwa. Na kwamba Mkakati umewekwa kumaliza madeni hayo katika muda mfupi uwezekanavyo kulingana na uzalishaji wa kampuni. Katika ziara hiyo Mwenyekiti Prof Kondoro alifuatana na Wajumbe wote wa Bodi wakiwemo Mama Martha maeda, Mama Mariam Mwanilwa. Wengine ni Mzee Linford Mboma, Mhandisi Cherles Mvungi, Mhandisi Karim mattaka na Mkurugenzi Mahamud Mabuyu. Aidha ziara hiyo walikuwepo Maafisa waandamizi wa TRL kadhaa.
Ziara hiyo ilianza Julai 14, 2017 Kigoma na kumalizika Mwanza Julai 18, 2017. Baadhi ya maeneo yalitembelewa na Bodi ni pamoja na Kigoma mjini, ikiwemo  ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bandari ya Kigoma na Stesheni ya Reli ya Kigoma. Aidha pia Bodi ilitembelea Mpanda Stesheni za  Katumba , Isaka, Shinyanga, Malya.
Jijini Mwanza Bodi ilipata fursa ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela. Baadae ujumbe ukatembelea bandari ya Mwanza Kaskazini na pia Mwanza Kusini na  kuhitimisha kwa kuzungumza na Wanareli wa Mwanza katika eneo la karakana. Ujumbe huo wa Bodi ulirejea Dar es salaam jioni Julai 18, 2017.

MWENYEKITI WA BODI PROFESA KONDORO AUNGANA NA WANARELI KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA NGAZI YA TAASISI !

MWENYEKITI WA BODI PROFESA KONDORO AUNGANA NA WANARELI KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA NGAZI YA TAASISI !

Juni 02, 2017, asubuhi, Mwenyekiti wa Bodi ya TRL Profesa John Wajanga Kondoro akifuatana na Mjumbe wa Bodi Mhandisi Charles Mvungi walishirikiana na Wanareli katika Kituo kikuu cha Reli cha Dar es Salaam kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani ngazi ya taasisi kwa kusafisha maeneo yote ya kituo hicho. Habari zaidi katika picha……MWENYEKITI MAZINGIRA 3

MWENYEKITI MAZINGIRA 2

MWENYEKITI MAZINGIRA 4

MWENYEKITI MAZINGIRA 5

MWENYEKITI MAZINGIRA 6

MWENYEKITI MAZINGIRA 7

MWENYEKITI MAZINGIRA 8

MWENYEKITI MAZINGIRA 9

MWENYEKITI MAZINGIRA 10

MWENYEKITI MAZINGIRA 11

MWENYEKITI MAZINGIRA 12

MWENYEKITI MAZINGIRA 13

MWENYEKITI MAZINGIRA 15

MWENYEKITI MAZINGIRA 16

MWENYEKITI MAZINGIRA 18

MWENYEKITI MAZINGIRA 19

MWENYEKITI MAZINGIRA 20

WANARELI WATAKIWA KUBADILIKA KATIKA UTENDAJI WAO WA KAZI!

posted in: Events, Media, Press Release | 0
ziara ya bodi 35
Mwenyekiti wa Bodi Profesa John Wajanga Kondoro akzungumza na Wnareli wa Dododma hivi karibuni

 

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Profesa John Wajanga Kondoro amewataka Wanareli kuacha kufanya kazi kwa mazoeya na badala yake wajiongeze ili kukabiliana na changamoto za ushindani  katika biashara ya usafirishaji nchini.

Ujumbe huu amekuwa akiutoa wakati wa mazungumzo yake na Wanareli  wa Tabora, Dodoma na Morogoro katika ziara ya kujitambulisha ya Bodi ya TRL ilioanza Machi 01 Tabora na kumalizika Machi 05, 2017 Dar es Salaam.. 

ziara ya bodi 10
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa akizungumza na Wanareli wa Karakana Kuu ya Morogoro Machi 4, 2017

 

 

Wito huo .Mwenyekiti wa Bodi alikuwa anautoa kila baada kusikiliza michango ya mawazo ya wanareli na kero zao kikazi na kimaslahi..

Amesema kuwa Bodi ni kiungo baina ya Wafanyakazi, Menejimenti na mwenye mali ambayo ni Serikali. Alitoa wito kwa Wanareli kuendelea kutoa ushirikiano kwa Menejimenti na pia kuitaka Menejimenti ikiongozwa na Nd Masanja Kadogosa kuendelea kutatua kero za Wanareli zile zilizo ndani ya uwezo wake.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji Nd Kadogosa amebainisha kuwa Uongozi wa TRL tayari imeshalipa jumla ya Shilingi bilioni 7.1 ikiwa ni malimbikizo ya madeni  kati ya Julai , 2016 hadi Februari , 2017. Malipo yalihusu michango katika hifadhi za jamii ikiwemo Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF). Pia ilidhihirika katika malimbikizo ya nyongeza  ya mshahara nyongeza 3 zimeshalipwa katika ya 5 na hivyo kubakia na deni la nyongeza 2 tu.

Baadhi ya kero zilizoainishwa .katika ziara hiyo ya Bodi ambayo ilihusu kujua matatizo ya miundo mbinu  na kero za wanareli ni pamoja na kero za maji magengeni, Wanareli kuwepo katika ngazi moja ya Utumishi  kwa    

 

 zaidi ya miaka kati ya 10 hadi 20

Profesa Kondoro aliwaahidi Wanareli wa mikoani kero zao zitakuwa ajenda muhimu katika vikao vijavyo vya Bodi na kusisitiza kuwa wawe wabunifu na kuhimizana kuchapa kazi kwa bidii na kutowavumilia wenzao wachache wanaoshiriki katika vitendo vya hujuma.

 

ziara ya bodi 8
Mwenyekiti wa Bodi Profesa John Wajanga Kondoro akizungumza na Wanareli wa Karakana Kuu ya Morogoro hivi karibuni

 

 

ziara ya bodi
Wanareli wa Karakana Kuu Morogoro wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya TRL Profesa John Kondoro Machi 04, 2017

 

 

 

Mwanareli wa Dodoma akitoa maoni yake katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi Machi 03, 2017 .

MKUTANO WA WANARELI NA VIONGOZI WA TRAWU NA WATAALAM WA TIB KATIKA PICHA !

posted in: Events, Media | 0

MKUTANO WA WANARELI NA VIONGOZI WA TRAWU NA WATAALAM WA TIB KARAKANA YA DAR JANUARI 02, 2017 ..KATIKA PICHA

 

 

trawu13
Wanareli waklisikiliza kwa makini Watoa hoja katika mkutano wa Trawu ,TIB na WSafanyakazi wa TRL uliofanyika Karakana ya Dar Januari 02, 2017.

 

 

trawu
Mtaalamu mmojawapo wa semina y mikopo ya TIB  akielezea bidhaa mbali mbali za mikopo ambazo benki ya TIB iko tayari kuwapatia Wanareli baada ya kukamilisha utaratibu rasmi.
trawu09
Kiongozi mzoefu wa Trawu TRL Nd Sheikh Shughuli akiwatambulisha viongozi wapya wa Trawu Taifa wakiwemo Mwenyekiti Nd Ole Saitabau
trawu03
Mtaalamu mmojawapo wa semina ya mikopo ya TIB akielezea bidhaa mbali mbali za mikopo ambazo benki ya TIB iko tayari kuwapatia Wanareli baada ya kukamilisha utaratibu rasmi.
trawu05
Mwanareli Athuman Kupaza akichangia hoja ya ya bidhaa za kibenki za TIB kwa Wanareli..
trawu-01
Makamu Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Trawu Taifa Nd Elizabeth Msewma akisalimia na Wanareli wakati wa kikao maalum cha kuwatambulisha Viongozi wapya Trawu Taifa kilichofanyika Karakana Dar Januari 02, 2017
trawu06
Mwanareli Temba akitoa hoja zake wakati wa mkutano
trawu07
Viongozi wapya wa Trawu Taifa wakisubiri kutambulishwa
trawu13a
Mwenyekiti mpya wa Trawu ngazi ya Taifa Nd Ole Saitabau akiwasalimia Wanareli ..
trawu12a
Makamu Mwenyekiti wa Trawu Taifa Nd Yusuf Mandia akisalimia Wanareli.
trawu11a
Katibu Mkuu wa Trawu Taifa Nd Christopher Kaziyo akiwasalimia Wanareli..

 

 

trawu11
Mwenyekiti Mstaafu wa Trawu Taifa Nd Mussa Kalala akiwasalimia na kuwaaga Wanareli wa TRL

 

 

trawu4
Wanareli wakifuatilia kwa makini mkutano wa Januari 02, 2017 uliofanyika Karakana ya Dar es Salaam.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

TRENI YA ABIRIA YAINGIA KITUO CHA DAR ‘RIGHT TIME’ JULAI 23, 2016!

Maboresha yanayoendelea ndani ya TRL ambayo yanatokana na uwekezaji endelevu wa vitendea kazi unaofanywa na Serikali  na ukarabarti wa njia unaanza kuzaa matunda ikiwemo hususan treni za abiria kukufika mwisho wa safari kwa wakati.

Ushuhuda wa kauli hii ni treni ya abiria kutoka Kigoma na Mwanmza iliondoka saa 11 jioni Kigoma na saa 12 jioni Mwanza iliwasili kituo kikmuu cha Dar es Salaam kwa wakati rasmi yaani saa 6:10 mchana Jumamosi Julai 23, 2016.Hali ya kuja kwa lugha ya kireli ‘right on time’ ilimshqawishi Kaimu Mkurugenzui Mtendani Nd Focus Sahani kuja kuipokea treni hiyo na kumpongeza dereva wake Ndugu Kessy Linden kwa niaba ya madereva wa Kigoma, Mwanza, Tabora, Dodoma. Shime Wanareli tuzidi kuongeza bidii na maarifa haki ya Mungu ..tutatoka tu na HAPA KAZI TU!SAM_0546 SAM_0543 SAM_0536 SAM_0537 SAM_0534 SAM_0552 SAM_0555 SAM_0567 SAM_0566