HUDUMA YA TRENI YA PUGU AWAMU ZOTE KUWA NA SAFARI 3 KUANZIA MACHI 27, 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
 
 
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) unawatangazia watumiaji wa huduma ya treni ya Jiji iendayo Pugu kuwa kuanzia Jumatatu Machi 27, 2017 ratiba yake ya kawaida ya safari 3 kwa awamu ya asubuhi na alasiri itaanza tena.
 
Taarifa imeainisha kuwa kazi ya kutandika reli nzito ratili 80 imekamilika kwa asilimia 75 tokea ilipoanza pale Januari 03, mwaka huu wa 2017. Kati ya vituo vya reli vya Dar es salaam na Pugu ni kuna umbali wa kilomita 20.
 
Safari ya treni kutoka kituo cha Pugu kwenda kituo Kikuu cha Dar es Salaam kwa awamu ya asubuhi ya kwanza itaondoka saa 12 asubuhi juu ya alama ya pili saa 2:10 na ya tatu saa 4:20.
Aidha jioni treni ya kwanza itaondoka Kituo Kikuu cha Dar kwenda Pugu saa 9::55 alasiri, ya pili saa 12:05 magharibi na ya tatu ambayo ni ya mwisho itaondoka saa 2:15 usiku. Atakayesoma taarifa hii amuarifu na mqwenzake.
 
Uongozi wa TRL unawashukuru sana wateja wake wa Pugu kwa kwa ushirkiano walioutoa katika kipindi chote cha uakarabati wa reli kati ya Kituo Kikuu cha Dar es Salaam na cha Pugu.
 
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Nd. Masanja Kadogosa,
Dar es Salaam,
Machi 25, 2017.1909700_10209313935753670_1272537156472894348_n

WANARELI WATAKIWA KUBADILIKA KATIKA UTENDAJI WAO WA KAZI!

posted in: Events, Media, Press Release | 0
ziara ya bodi 35
Mwenyekiti wa Bodi Profesa John Wajanga Kondoro akzungumza na Wnareli wa Dododma hivi karibuni

 

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Profesa John Wajanga Kondoro amewataka Wanareli kuacha kufanya kazi kwa mazoeya na badala yake wajiongeze ili kukabiliana na changamoto za ushindani  katika biashara ya usafirishaji nchini.

Ujumbe huu amekuwa akiutoa wakati wa mazungumzo yake na Wanareli  wa Tabora, Dodoma na Morogoro katika ziara ya kujitambulisha ya Bodi ya TRL ilioanza Machi 01 Tabora na kumalizika Machi 05, 2017 Dar es Salaam.. 

ziara ya bodi 10
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa akizungumza na Wanareli wa Karakana Kuu ya Morogoro Machi 4, 2017

 

 

Wito huo .Mwenyekiti wa Bodi alikuwa anautoa kila baada kusikiliza michango ya mawazo ya wanareli na kero zao kikazi na kimaslahi..

Amesema kuwa Bodi ni kiungo baina ya Wafanyakazi, Menejimenti na mwenye mali ambayo ni Serikali. Alitoa wito kwa Wanareli kuendelea kutoa ushirikiano kwa Menejimenti na pia kuitaka Menejimenti ikiongozwa na Nd Masanja Kadogosa kuendelea kutatua kero za Wanareli zile zilizo ndani ya uwezo wake.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji Nd Kadogosa amebainisha kuwa Uongozi wa TRL tayari imeshalipa jumla ya Shilingi bilioni 7.1 ikiwa ni malimbikizo ya madeni  kati ya Julai , 2016 hadi Februari , 2017. Malipo yalihusu michango katika hifadhi za jamii ikiwemo Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF). Pia ilidhihirika katika malimbikizo ya nyongeza  ya mshahara nyongeza 3 zimeshalipwa katika ya 5 na hivyo kubakia na deni la nyongeza 2 tu.

Baadhi ya kero zilizoainishwa .katika ziara hiyo ya Bodi ambayo ilihusu kujua matatizo ya miundo mbinu  na kero za wanareli ni pamoja na kero za maji magengeni, Wanareli kuwepo katika ngazi moja ya Utumishi  kwa    

 

 zaidi ya miaka kati ya 10 hadi 20

Profesa Kondoro aliwaahidi Wanareli wa mikoani kero zao zitakuwa ajenda muhimu katika vikao vijavyo vya Bodi na kusisitiza kuwa wawe wabunifu na kuhimizana kuchapa kazi kwa bidii na kutowavumilia wenzao wachache wanaoshiriki katika vitendo vya hujuma.

 

ziara ya bodi 8
Mwenyekiti wa Bodi Profesa John Wajanga Kondoro akizungumza na Wanareli wa Karakana Kuu ya Morogoro hivi karibuni

 

 

ziara ya bodi
Wanareli wa Karakana Kuu Morogoro wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya TRL Profesa John Kondoro Machi 04, 2017

 

 

 

Mwanareli wa Dodoma akitoa maoni yake katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi Machi 03, 2017 .

SALAAM ZA MWAKA MPYA WA 2017 KWA WANARELI KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL ND. MASANJA KUNGU KADOGOSA

SALAAM ZA MWAKA MPYA WA 2017 KWA WANARELI KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL

ND. MASANJA KUNGU KADOGOSA

 

 

Nd Masanja Kadogosa


Ndugu Wanareli Wenzangu;

Nawatakia Mwaka mpya 2017 mwema, kama nilivyotangulia kusema awali, Naamini 2017 utakuwa wa mafanikio makubwa kwenye sekta ndogo hii ya Reli, kila mmoja wetu atimize wajibu hapo alipo, kabla ya kunyoshea kidole mwenzako, jiulize kwanza uwepo wako na unachokifanya kinaharakisha kuyafikia yale 

Wanarelii wote tumedhamiria. Tumefanya mengi 2016, tunakila sababu ya kujipongeza na kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi Rehema. Hata hivyo ni vyema tukafahamu adui wa kwanza katika uongozi ni yale mafanikio ya mwisho, ni rahisi uongozi kujisahau na kuzani kila jambo linaenda vyema, mwaka 2017 tutazikabili changamoto zetu kwa nguvu zote, dhamira ya uongozi ni kuona wafanyakazi wetu wanaishi kama wafanyakazi wengine kwenye taasisi za serikali. Kwa pamoja haya yote yanawezekana.

Wasalaam ,

MASANJA KUNGU KADOGOSA

MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL

Waziri Mkuu Atembelea Kiluwa Steel Groupe kujionea miundo mbinu ya reli!

posted in: Media, Press Release | 0
ZIARA YA MHE WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KATIKA KIWANDA CHA BIDHAA ZA CHUMA CHA KILUWA GROUP MLANDIZI LEO ASUBUHI NOVEMBA 19, 2016 KATIKA PICHA.
trl-pm-3
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa pamoja na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakimsikiliza Taarfia ya Mtendaji Mkuu wa TRL
trl-pm-5
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa akitoa taarifa fupi ya TRL kwa Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa

 

 

trl-pm-1
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa taarifa fupi kwa Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa kuhusu maendeleo ya Kiluwa Steel Groupe Mlandizi
Pamoja na mambo mengi Mhe Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifika kiwandani hapo kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa mwezi Julai , 2016 kuhusu upatikanaji wa mchepuo wa njia ya reli ndani ya kiwanda na umeme wa msongo mkubwa wa Tanesco.
Mhe Waziri Mkuu alifurahi kuthibitisha kwa macho yake kuwa tayari njia ya reli yenye urefu wa kilomita 4.6 imeshatandikwa na kushuhudia kichwa cha treni kikivuta mabehewa kikitembea katika reli hiyo.
Waziri Mkuu alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa na Wafanyakazi wa TRL kwa kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha agizo lake linatakelezwa kwa vitendo.
Aidha alisema Serikali iko katika mchakato wa kuziunganisha taasisi za Rahco na TRL ili zifanye kazi kwa ufanisi na kuleta tija katika maendelea ya Taifa kwa jumla.
 
Alisisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuboresha huduma za reli kwa kujenga reli ya kisasa ya kiwango cha ‘standard gauge’ na kwamba hivi karibuni Mkandarasi wa awamu ya kwanza atapatikana kuanza kazi hiyo.
 
Kuhusu upatikanaji wa Umeme mkubwa Waziri Mkuu alifurahi kwa kutaarifiwa kuwa Tanesco tayari imeshaleta njia ya umeme wa msongo mkubwa na kwamba mchakato wa majaribio ukikamilika umeme huo utakuwa tayari kutumika kiwandani hapo mnamo Desemba 07, 2016.
 
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alimkaribisha Waziri Mkuu kiwandani hapo na kutoa taarifa fupi akifuatiwa na Mtendaji Mkuu wa TRL, Mtendaji Mkuu wa Kiluwa Steel Works Group na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda.
trl-pm-6trl-pm-8
trl-pm-7
 trl-pm-9 trl-pm-10 trl-pm-11 trl-pm-12 trl-pm-13 trl-pm-14 trl-pm-15
trl-pm-17 trl-pm-18 trl-pm-19

Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Picha

posted in: Media, Press Release | 0
trl-bkw-6
Mkurugenzi Mtendaji TRL Nd Masanja Kadogosa akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TRL uliofanyika katika ukumbi wa Kitengo cha Zimamoto cha TPA jijini Novemba 17 na 18 ,2016
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa amefungua mkutano wa siku mbili wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TRL katika ukumbi mikutano wa kitengo cha Zimamoto cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) bendera tatu jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine umejadili  mikakati ya kuzipatia ufumbuzi  changamoto zote zinazoikabili TRL katika jitihada za kuondoka katika hali ya utendaji duni na kuwa taasisi yenye ufanisi katika utoaji huduma za usafirishaji wa reli nchini.
Aidha mkutano wa Baraza Kuu unatarajiwa kutoa maazimio ya kuboresha maslahi ya Wanareli kwa ujumla na kuimarisha utendaji kazi kwa moyo wa kizalendo, uadilifu na kujituma zaidi.
Maandalizi ya kuziunganisha TRL na Rahco kumefanya mkutano kufanyika katika mazingira ya utulivu na matumaini makubwa. Mkutano umejadi pamoja na mambo mengine taarifa ya kazi ya udhibiti wa mafuriko kati ya maeneo ya stesheni za Gulwe, Kidete na Kilosa.
li trl-bkw-3 trl-bkw-5trl-bkw-4   trl-bkw-8  trl-bkw7trl-bwk-2   trl-bkw-9

UZINDUZI WA BODI KATIKA PICHA

posted in: Media, Press Release | 0

 

UZINDUZI WA BODI YA MPYA TRL KATIKA PICHA  ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO  MAKAO MAKUU YA TRL NOVEMBA 16, 2016!
trl-uzinduzi-wa-bodi-mkk-10
Waziri wa UJenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mnyaa Mbarawa akimkabidhi tablet kama kitendea kazi  Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TRL Profesa John Kondoro siku ya uzinduzi wa Bodi Novemba 16, 2016
trl-uzinduzi-wa-bodi-mkk-1
Mkurugenzi Mtendaji Nd. Masanja Kadogosa akisoma taarifa wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya TRL Novemba 16, 2016
trl-uzinduzi-wa-bodi-mkk-2
Wajumbe wa Bodi Bibi Martha Maeda na Bw Linford Mboma wakisikiliza kwa makini nasaha za mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya TRL. .
trl-uzinduzi-wa-bodi-mkk-5
Msajili wa Hazina Bw Lawrence Mafuru akitoa nasaha zake kwa Wajumbe wa Bodi mpya ya TRL.

 

Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akitoa nasaha zake kwa Wajumbe wa Bodi mpya ya TRL wakati wa hafla ya uzinduzi.
trl-uzinduzi-wa-bodi-mkk-11
Bwana Linford Mboma ( Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa lilikuwa Shirika la Reli nchini na pia Mtendaji wa kwanza wa Rahco akijtambulisha kwa mgeni rasmi
trl-uzinduzi-wa-bodi-mkk-12
Mtendaji Mkuu wa TRL Nd Masanja Kadogosa akimkabidhi kwa niaba ya mgeni rasmi mkoba wenye makabrasha Mjumbe wa Bodi Bw Linford Mboma
trl-uzinduzi-wa-bodi-mkk-13
Waziri wa UJenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mnyaa Mbarawa akimkabidhi mkoba wenye makabrasha Mjumbe wa Bodi mpya ya TRL Bibi Martha Maeda (TIB);

trl-uzinduzi-wa-bodi-mkk-3

ORODHA RASMI YA BODI MPYA YA TRL NI KAMA IFUATAVYO:
Mwenyekiti ni Profesa John Wajanga Kondoro( Mkuu wa Chuo Mstaafu wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT);
Bwana Linford Mboma ( Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa lilikuwa Shirika la Reli nchini na pia Mtendaji wa kwanza wa Rahco);
Bibi Miriam G. Mwanilwa kutoka Ofisi ya Rais , Bodi ya Mishahara.
Wengine ni Bibi Martha Maeda (TIB); Mhandisi Charles C.N.Mvungi(TIB) na Mahamoud Mashaka Mabuyu (WFP). Waziri Mbarawa alianisha jana kuwa atamteua hivi karibuni mjumbe wa saba wa bodi hiyo kutoka Mamlaka ya Bandari nchini TPA.

 

TRENI YA 3 YA ABIRIA YA KAWAIDA KUANZA JUMAPILI SEPTEMBA 04, 2016

SAM_0536KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)

(TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)
TRL YAFANYA MABADILIKO YA RATIBA YA SAFARI ZA ABIRIA KWENDA BARA NA KUONGEZA MOJA KUANZIA SEPTEMBA 01 , 2016

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umeamua kuongeza safari ya tatu ya treni ya abiria ya kawaida kwenda bara ambayo itaondoka Dar es Salaam kila Jumapili, safari ya kwanza itakuwa Jumapili hii ya Septemba 04, 2016 saa 9 alasiri.

Taarifa imeainisha kuwa treni hiyo ya huduma ya kawaida itakuwa na mabehewa 12 kutokea Dar es Salaam ikiwa na mabehewa manane ya daraja la 3, mawili daraja la pili kulala na mawili daraja la kwanza. Katika stesheni za Morogoro na Dodoma yataongezwa mabehewa mawili mawili ya daraja la 3.
Aidha treni ya Deluxe imebadilishwa siku ya kuondoka badala ya Jumapili kwa sasa kuanzia Septemba Mosi, 2016 itakuwa inaondoka siku ya Alhamis saa 2 asubuhi kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam.

Halikadhalika mabadiliko haya pia yataongeza safari za treni ya kwenda Mpanda kutoka Tabora badala ya 2 za sasa zitakuwa 3 kwa wiki ambazo ni Jumatatu, Jumatano na Jumamosi..
Wakati huohuo Uongozi wa TRL umefanya uamuzi wa kihistoria wa kupeleka huduma za kuuzwa tiketi za safari zake mjini Kasulu ambapo kuanzia Septemba Mosi itafungua kituo cha Reli ambacho kitafanya kazi ya kuto huduma hiyo kwa wasafari wanaotoka Kasulu mjini na maeneo ya jirani . Kwa uamuzi huo TRL imetoa nafasi za tiketi za behewa moja la daraja la 3. Mpango pia uko mbioni wa kufungua kituo kama hicho siku zijazo mjini Kibondo hali itakaporuhusu kulingana na mahitaji halisi ya abiria.

Taarifa imesisitiza kuwataka wasafiri na wananchi kwa jumla nchini hususan wale wa Mpanda na Kibondo kutumia fursa ya kuongezewa safari na huduma kuletewa karibu kwa kufuata sheria , taratibu na kanuni ili hatua iliyochukuliwa na TRL iwe na tija iliokusudiwa.
Aidha taarifa zaidi zinaarifu kuwa hatimaye TRL imefanikiwa kuongeza mabehewa mawili zaidi ya treni ya Pugu na kufikia idadi ya behewa 18 hadi jana Agosti 22, 2016. Ni matarajio ya Uongozi ifikapo Agosti 31, 2016 treni hiyo ya Jiji itakuwa na mabehewa 20 iloahidi ili kupunguza msongamano unaosababishwa na abiria kuwa wengi katika safari mbili za awali katika awamu zote 2 ya asubuhi na ya jioni.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Focus Makoye Sahani,
Dar es Salaam,
Agosti 23, 2016.1909700_10209313935753670_1272537156472894348_n

ABIRIA YA BARA KUONDOKA SAA 9 ALASIRI NA TRENI YA PUGU KUANZA AGOSTI MOSI!

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)

 

     

 

 

(TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)

KUBADILISHWA MUDA WA KUONDOKA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA KUANZIA AGOSTI  02 ,  2016!

 

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) unatangazwa kubadilishwa muda wa kuondoka treni ya abiria kutoka Dar es Salaaam kwenda bara kuanzia Agosti 02, 2016, ambapo treni  itaondoka saa 9 alasiri ri badala ya saa 11 jioni iliozoeleka. Kutokana na mabadiliko hayo abiria wanatakiwa kufika kituo Kikuu cha reli Dar es Salaam mapema saa 7 mchana.

 

Mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa treni ya pili ya huduma ya Jiji kutoka kituo kikuu  cha reli cha  Dar es Salaam kwenda Pugu ambayo itaanza kutoa huduma Jumatatu Agosti Mosi, 2016.

 

Aidha taarifa ya Menejimenti imefafanua kuwa  mabadiliko hayo yanahusu treni za abiria za huduma ya kawaida zinaondoka siku za Jumanne na Ijumaa. Hata hivyo huduma ya treni ya deluxe itaondoka muda wake wa kawaida kila Jumapili kwenda Kigoma saa 2 asubuhi.

 

Kuhusu huduma ya pili ya treni ya Jiji kwenda Pugu taarifa imefafanua kuwa huduma hiyo itakuwa na vituo 10 vifuatavyo: Pugu Stesheni,  Mwisho wa lami, Gongo la mboto, FFU Mombasa, Banana( njia panda kwenda Segerea), na Karakata. Vingine ni pamoja na Vingunguti Mbuzi, SS Bakhressa, Kamata na Kituo kikuu cha reli Dar es Salaam.

 

Huduma ya treni hiyo itakuwa ya awamu mbili asubuhi na Alasiri ambapo treni ya kwanza itaondoka kituo cha Pugu saa 12 asubuhi na kuwasili kituo cha Dar es Salaam saa 12:55 asubuhi na kufanya safari 3 zitakazomalizika saa 05:15 asubuhi. Jioni pia kutakuwa na safari 3  ambapo treni ya kwanza  itaondoka kituo cha Dar es Salaam saa 09:55 alasiri kwenda Pugu  na kuwasili saa 10:50 jioni na safari ya mwisho kutoka Pugu kuja Dar itakuwa saa 03:20 usiku.

 

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :

Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,

Nd Masanja Kungu Kadogosa,

Dar es Salaam,

Julai 29, 2016.1909700_10209313935753670_1272537156472894348_n1909700_10209313935753670_1272537156472894348_n

TRENI YA ABIRIA YAINGIA KITUO CHA DAR ‘RIGHT TIME’ JULAI 23, 2016!

Maboresha yanayoendelea ndani ya TRL ambayo yanatokana na uwekezaji endelevu wa vitendea kazi unaofanywa na Serikali  na ukarabarti wa njia unaanza kuzaa matunda ikiwemo hususan treni za abiria kukufika mwisho wa safari kwa wakati.

Ushuhuda wa kauli hii ni treni ya abiria kutoka Kigoma na Mwanmza iliondoka saa 11 jioni Kigoma na saa 12 jioni Mwanza iliwasili kituo kikmuu cha Dar es Salaam kwa wakati rasmi yaani saa 6:10 mchana Jumamosi Julai 23, 2016.Hali ya kuja kwa lugha ya kireli ‘right on time’ ilimshqawishi Kaimu Mkurugenzui Mtendani Nd Focus Sahani kuja kuipokea treni hiyo na kumpongeza dereva wake Ndugu Kessy Linden kwa niaba ya madereva wa Kigoma, Mwanza, Tabora, Dodoma. Shime Wanareli tuzidi kuongeza bidii na maarifa haki ya Mungu ..tutatoka tu na HAPA KAZI TU!SAM_0546 SAM_0543 SAM_0536 SAM_0537 SAM_0534 SAM_0552 SAM_0555 SAM_0567 SAM_0566

1 2