HUDUMA YA TRENI ZA ABIRIA NA MIZIGO KUHAMISHIWA MOROGORO KUANZIA KESHO!

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)

 

     

 

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI –PRESS RELEASE

 SAM_0537

HUDUMA YA TRENI ZA ABIRIA NA MIZIGO  KUANZIA MOROGORO HAPO KESHO JUMAMOSI MEI 20, 2017

 

Uongozi  Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kuhamishia kwa muda huduma ya usafiri wa treni kwenda bara katika kituo cha Morogoro kuanzia kesho Jumamosi Mei 20, 2017, badala ya  Dar es Salaam. Abiria watakaohusika ni wale wenye tiketi waliokuwa waondoke leo  Ijumaa na wale wa Jumapili ambao treni zao zimefutwa.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya TRL abiria wanatakiwa wafike kituo kikuu cha Reli Dar es Salaam kesho Jumamosi  kabla ya .saa  Moja asubuhi ambapo watasafirishwa kwa mabasi maalum yaliyokodiwa na TRL hadi Morogoro ambako watapanda  treni kwenda bara itakayoondoka  saa Moja kamili usiku.

 

Kuhusu Wafanya biashara  wasafirishaji wa shehena kwenda bara wametakiwa kuwasiliana na Idara ya masoko ya TRL ili kupewa utaratibu wa jinsi ya kusafirisha mizigo yao hadi Morogoro ambako itasafirishwa kwa treni kwenda bara.

Uamuzi huu umechukuliwa kufuatia kipande cha reli kati ya Dar es Salaam na Ruvu kuwa hakipitiki baada ya daraja la reli la Ruvu kutitia upande mmoja

 

Mamlaka husika zinafanyia kazi ukarabati wa daraja hilo ili njia ya reli kutoka hadi Morogoro  ifunguliwa kwa muda mfupi iwezekanavyo.

 

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya TRL Profesa John Kondoro na wajumbe wengine wa Bodi asubuhi hii wametembelea eneo la daraja ambapo walifanya tathmini na  Bodi kama mamlaka ilitoa  maelekezo yake kwa Menejimenti ya TRLi  kuhusu maandalizi  na utekelezaji wa  kazi za ukarabati wa daraja hilo..

 

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:

Kwa Niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KampunI ya Reli Tanzania(TRL),

Ndugu Focus Makoye Sahani,

Mei 19, 2017

DAR ES SALAAM

SAFARI ZA TRENI KWENDA BARA ZASITISHWA KUANZIA LEO MEI 18, 2017

 

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)

 

     

 

                                                                 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI –PRESS RELEASE

 

KUSIMAMISHWA HUDUMA YA TRENI ZA ABIRIA KWENDA BARA KUANZIA LEO MEI 18, 2017

 

Uongozi  Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusimamishwa huduma ya treni za abiria kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuanzia leo Mei 18, 2017 hadi itakapotangazwa tena.

 

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kutokea uharibifu wa miundombinu ya reli leo asubuhi kati ya stesheni za Ruvu na Ruvu junction uliosababishwa na mvua kubwa zinazonyeshwa maeneo hayo ya mkoa wa Pwani.

 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo  ya kusitisha huduma kwa muda treni ya abiria ya deluxe iliokuwa iondoke Dar es Salaam leo saa 2 asubuhi imefutwa na abiria wametakliwa wafike stesheni ili warejeshewe fedha zao za nauli.

 

Wakati huo huo Uongozi wa TRL tayari umeelekea eneo la tukio ili kufanya tathmini na kupanga mikakati ya haraka kukarabati miundo mbinu husika likiwemo daraja la Ruvu.

 

Aidha Uongozi umefafanua katika taarifa yake kuwa katika kipindi cha mpito, treni ya abiria kutoka Kigoma na Mwanza kuja Dar es Salaam itaishia Morogoro hadi njia ya reli  kati ya Dar es Salaam na Morogoro  itakapofunguliwa tena.

 

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:

KampunI ya Reli Tanzania(TRL),

Mei 18, 2017

DAR ES SALAAM 

Treni ya Deluxe picha ya maktaba TRL
Treni ya abiria ya  Deluxe ikiwa Stesheni ya Morogoro picha ya maktaba TRL

UONGOZI WA TRL WAMEZINDUA HUDUMA  MAALUM YA USAFIRISHAJI SHEHENA WA ‘BLOCK TRAIN KWENDA BURUNDI MACHI 31, 2017 KUTOKA MALINDI YARD BANDARINI.

burundi block train 1
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  wa TRLNd Shaban Kiko akipunga bendera kuashiria kuazna safari ya ‘block trani’ yenye mzigo wa mteja wetu UBUCOM kutoka Burundi hapo Machi 31, 2017 Malindi Yard bandarini Dar es Salaam.

 

 

Imefahamika kuwa  huduma maalum ya usafirishaji shehena wa treni nzima ‘block train’ imezinduliwa rasmi na Uongozi  wa TRL kwenda Burundi katika  kituo cha Malindi bandarini Dar es Salaam Machi 31, 2017.

 

Huduma ya block train iliozinduliwa ni maalum kwa wafanyabiashara na kampuni binafsi  wenye  shehena  kubwa za mizigo kutosheleza mabehewa 20 ambapo hurahisisha kuisafirisha moja kwa moja hadi kwa mpokeaji( mwenye mzigo).

 

Kwa mujibu wa taarifa ya Uongozi wa TRL treni hiyo yenye mabehewa 20 imebeba malighafi ya chuma( iron coils) mzigo unaosafirishwa na Kampuni ya UBUCOM ya Burundi na utachukua muda wa siku 3 kuwasili Kigoma na siku moja kuwasili mjini Bujumbura. Burundi.

 

Aidha taarifa zaidi zimeainisha kuwa TRL imepunguza gharama za usafirishaji wa mizigo ya kawaida (loose cargo) na ile iliohifadhiwa katika makasha kwenda Burundi. Hivi sasa TRL inatoza jumla ya Dola za Kimarekani (USD)3,056 kwa behewa moja la mizigo ya kawaida na USD 3024/= kwa mizigo iliofungwa katika makasha hadi Bujumbura Burundi ikilinganishwa na  gharama ya  USD 3500/= ikisafirishwa barabarani.

Gharama za TRL zinahusisha pia  uhudumiaji shehena bandarini  Dar es Salaam, Kigoma na Bujumbura na pia usafiri wa reli hadi Kigoma na wa meli hadi Bujumbura.

burundi block train
Mandhari ya Kituo cha Malindi wakati ‘block train’ ya Burundi ikijitayarisha kuondoka Ijuumaa Machi 31, 2017

 

 

HUDUMA YA TRENI YA PUGU AWAMU ZOTE KUWA NA SAFARI 3 KUANZIA MACHI 27, 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
 
 
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) unawatangazia watumiaji wa huduma ya treni ya Jiji iendayo Pugu kuwa kuanzia Jumatatu Machi 27, 2017 ratiba yake ya kawaida ya safari 3 kwa awamu ya asubuhi na alasiri itaanza tena.
 
Taarifa imeainisha kuwa kazi ya kutandika reli nzito ratili 80 imekamilika kwa asilimia 75 tokea ilipoanza pale Januari 03, mwaka huu wa 2017. Kati ya vituo vya reli vya Dar es salaam na Pugu ni kuna umbali wa kilomita 20.
 
Safari ya treni kutoka kituo cha Pugu kwenda kituo Kikuu cha Dar es Salaam kwa awamu ya asubuhi ya kwanza itaondoka saa 12 asubuhi juu ya alama ya pili saa 2:10 na ya tatu saa 4:20.
Aidha jioni treni ya kwanza itaondoka Kituo Kikuu cha Dar kwenda Pugu saa 9::55 alasiri, ya pili saa 12:05 magharibi na ya tatu ambayo ni ya mwisho itaondoka saa 2:15 usiku. Atakayesoma taarifa hii amuarifu na mqwenzake.
 
Uongozi wa TRL unawashukuru sana wateja wake wa Pugu kwa kwa ushirkiano walioutoa katika kipindi chote cha uakarabati wa reli kati ya Kituo Kikuu cha Dar es Salaam na cha Pugu.
 
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Nd. Masanja Kadogosa,
Dar es Salaam,
Machi 25, 2017.1909700_10209313935753670_1272537156472894348_n

WANARELI WATAKIWA KUBADILIKA KATIKA UTENDAJI WAO WA KAZI!

posted in: Events, Media, Press Release | 0
ziara ya bodi 35
Mwenyekiti wa Bodi Profesa John Wajanga Kondoro akzungumza na Wnareli wa Dododma hivi karibuni

 

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Profesa John Wajanga Kondoro amewataka Wanareli kuacha kufanya kazi kwa mazoeya na badala yake wajiongeze ili kukabiliana na changamoto za ushindani  katika biashara ya usafirishaji nchini.

Ujumbe huu amekuwa akiutoa wakati wa mazungumzo yake na Wanareli  wa Tabora, Dodoma na Morogoro katika ziara ya kujitambulisha ya Bodi ya TRL ilioanza Machi 01 Tabora na kumalizika Machi 05, 2017 Dar es Salaam.. 

ziara ya bodi 10
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa akizungumza na Wanareli wa Karakana Kuu ya Morogoro Machi 4, 2017

 

 

Wito huo .Mwenyekiti wa Bodi alikuwa anautoa kila baada kusikiliza michango ya mawazo ya wanareli na kero zao kikazi na kimaslahi..

Amesema kuwa Bodi ni kiungo baina ya Wafanyakazi, Menejimenti na mwenye mali ambayo ni Serikali. Alitoa wito kwa Wanareli kuendelea kutoa ushirikiano kwa Menejimenti na pia kuitaka Menejimenti ikiongozwa na Nd Masanja Kadogosa kuendelea kutatua kero za Wanareli zile zilizo ndani ya uwezo wake.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji Nd Kadogosa amebainisha kuwa Uongozi wa TRL tayari imeshalipa jumla ya Shilingi bilioni 7.1 ikiwa ni malimbikizo ya madeni  kati ya Julai , 2016 hadi Februari , 2017. Malipo yalihusu michango katika hifadhi za jamii ikiwemo Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF). Pia ilidhihirika katika malimbikizo ya nyongeza  ya mshahara nyongeza 3 zimeshalipwa katika ya 5 na hivyo kubakia na deni la nyongeza 2 tu.

Baadhi ya kero zilizoainishwa .katika ziara hiyo ya Bodi ambayo ilihusu kujua matatizo ya miundo mbinu  na kero za wanareli ni pamoja na kero za maji magengeni, Wanareli kuwepo katika ngazi moja ya Utumishi  kwa    

 

 zaidi ya miaka kati ya 10 hadi 20

Profesa Kondoro aliwaahidi Wanareli wa mikoani kero zao zitakuwa ajenda muhimu katika vikao vijavyo vya Bodi na kusisitiza kuwa wawe wabunifu na kuhimizana kuchapa kazi kwa bidii na kutowavumilia wenzao wachache wanaoshiriki katika vitendo vya hujuma.

 

ziara ya bodi 8
Mwenyekiti wa Bodi Profesa John Wajanga Kondoro akizungumza na Wanareli wa Karakana Kuu ya Morogoro hivi karibuni

 

 

ziara ya bodi
Wanareli wa Karakana Kuu Morogoro wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya TRL Profesa John Kondoro Machi 04, 2017

 

 

 

Mwanareli wa Dodoma akitoa maoni yake katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi Machi 03, 2017 .

MKUTANO WA WANARELI NA VIONGOZI WA TRAWU NA WATAALAM WA TIB KATIKA PICHA !

posted in: Events, Media | 0

MKUTANO WA WANARELI NA VIONGOZI WA TRAWU NA WATAALAM WA TIB KARAKANA YA DAR JANUARI 02, 2017 ..KATIKA PICHA

 

 

trawu13
Wanareli waklisikiliza kwa makini Watoa hoja katika mkutano wa Trawu ,TIB na WSafanyakazi wa TRL uliofanyika Karakana ya Dar Januari 02, 2017.

 

 

trawu
Mtaalamu mmojawapo wa semina y mikopo ya TIB  akielezea bidhaa mbali mbali za mikopo ambazo benki ya TIB iko tayari kuwapatia Wanareli baada ya kukamilisha utaratibu rasmi.
trawu09
Kiongozi mzoefu wa Trawu TRL Nd Sheikh Shughuli akiwatambulisha viongozi wapya wa Trawu Taifa wakiwemo Mwenyekiti Nd Ole Saitabau
trawu03
Mtaalamu mmojawapo wa semina ya mikopo ya TIB akielezea bidhaa mbali mbali za mikopo ambazo benki ya TIB iko tayari kuwapatia Wanareli baada ya kukamilisha utaratibu rasmi.
trawu05
Mwanareli Athuman Kupaza akichangia hoja ya ya bidhaa za kibenki za TIB kwa Wanareli..
trawu-01
Makamu Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Trawu Taifa Nd Elizabeth Msewma akisalimia na Wanareli wakati wa kikao maalum cha kuwatambulisha Viongozi wapya Trawu Taifa kilichofanyika Karakana Dar Januari 02, 2017
trawu06
Mwanareli Temba akitoa hoja zake wakati wa mkutano
trawu07
Viongozi wapya wa Trawu Taifa wakisubiri kutambulishwa
trawu13a
Mwenyekiti mpya wa Trawu ngazi ya Taifa Nd Ole Saitabau akiwasalimia Wanareli ..
trawu12a
Makamu Mwenyekiti wa Trawu Taifa Nd Yusuf Mandia akisalimia Wanareli.
trawu11a
Katibu Mkuu wa Trawu Taifa Nd Christopher Kaziyo akiwasalimia Wanareli..

 

 

trawu11
Mwenyekiti Mstaafu wa Trawu Taifa Nd Mussa Kalala akiwasalimia na kuwaaga Wanareli wa TRL

 

 

trawu4
Wanareli wakifuatilia kwa makini mkutano wa Januari 02, 2017 uliofanyika Karakana ya Dar es Salaam.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

SALAAM ZA MWAKA MPYA WA 2017 KWA WANARELI KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL ND. MASANJA KUNGU KADOGOSA

SALAAM ZA MWAKA MPYA WA 2017 KWA WANARELI KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL

ND. MASANJA KUNGU KADOGOSA

 

 

Nd Masanja Kadogosa


Ndugu Wanareli Wenzangu;

Nawatakia Mwaka mpya 2017 mwema, kama nilivyotangulia kusema awali, Naamini 2017 utakuwa wa mafanikio makubwa kwenye sekta ndogo hii ya Reli, kila mmoja wetu atimize wajibu hapo alipo, kabla ya kunyoshea kidole mwenzako, jiulize kwanza uwepo wako na unachokifanya kinaharakisha kuyafikia yale 

Wanarelii wote tumedhamiria. Tumefanya mengi 2016, tunakila sababu ya kujipongeza na kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi Rehema. Hata hivyo ni vyema tukafahamu adui wa kwanza katika uongozi ni yale mafanikio ya mwisho, ni rahisi uongozi kujisahau na kuzani kila jambo linaenda vyema, mwaka 2017 tutazikabili changamoto zetu kwa nguvu zote, dhamira ya uongozi ni kuona wafanyakazi wetu wanaishi kama wafanyakazi wengine kwenye taasisi za serikali. Kwa pamoja haya yote yanawezekana.

Wasalaam ,

MASANJA KUNGU KADOGOSA

MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL

Waziri Mkuu Atembelea Kiluwa Steel Groupe kujionea miundo mbinu ya reli!

posted in: Media, Press Release | 0
ZIARA YA MHE WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KATIKA KIWANDA CHA BIDHAA ZA CHUMA CHA KILUWA GROUP MLANDIZI LEO ASUBUHI NOVEMBA 19, 2016 KATIKA PICHA.
trl-pm-3
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa pamoja na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakimsikiliza Taarfia ya Mtendaji Mkuu wa TRL
trl-pm-5
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa akitoa taarifa fupi ya TRL kwa Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa

 

 

trl-pm-1
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa taarifa fupi kwa Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa kuhusu maendeleo ya Kiluwa Steel Groupe Mlandizi
Pamoja na mambo mengi Mhe Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifika kiwandani hapo kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa mwezi Julai , 2016 kuhusu upatikanaji wa mchepuo wa njia ya reli ndani ya kiwanda na umeme wa msongo mkubwa wa Tanesco.
Mhe Waziri Mkuu alifurahi kuthibitisha kwa macho yake kuwa tayari njia ya reli yenye urefu wa kilomita 4.6 imeshatandikwa na kushuhudia kichwa cha treni kikivuta mabehewa kikitembea katika reli hiyo.
Waziri Mkuu alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa na Wafanyakazi wa TRL kwa kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha agizo lake linatakelezwa kwa vitendo.
Aidha alisema Serikali iko katika mchakato wa kuziunganisha taasisi za Rahco na TRL ili zifanye kazi kwa ufanisi na kuleta tija katika maendelea ya Taifa kwa jumla.
 
Alisisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuboresha huduma za reli kwa kujenga reli ya kisasa ya kiwango cha ‘standard gauge’ na kwamba hivi karibuni Mkandarasi wa awamu ya kwanza atapatikana kuanza kazi hiyo.
 
Kuhusu upatikanaji wa Umeme mkubwa Waziri Mkuu alifurahi kwa kutaarifiwa kuwa Tanesco tayari imeshaleta njia ya umeme wa msongo mkubwa na kwamba mchakato wa majaribio ukikamilika umeme huo utakuwa tayari kutumika kiwandani hapo mnamo Desemba 07, 2016.
 
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alimkaribisha Waziri Mkuu kiwandani hapo na kutoa taarifa fupi akifuatiwa na Mtendaji Mkuu wa TRL, Mtendaji Mkuu wa Kiluwa Steel Works Group na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda.
trl-pm-6trl-pm-8
trl-pm-7
 trl-pm-9 trl-pm-10 trl-pm-11 trl-pm-12 trl-pm-13 trl-pm-14 trl-pm-15
trl-pm-17 trl-pm-18 trl-pm-19

Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Picha

posted in: Media, Press Release | 0
trl-bkw-6
Mkurugenzi Mtendaji TRL Nd Masanja Kadogosa akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TRL uliofanyika katika ukumbi wa Kitengo cha Zimamoto cha TPA jijini Novemba 17 na 18 ,2016
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa amefungua mkutano wa siku mbili wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TRL katika ukumbi mikutano wa kitengo cha Zimamoto cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) bendera tatu jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine umejadili  mikakati ya kuzipatia ufumbuzi  changamoto zote zinazoikabili TRL katika jitihada za kuondoka katika hali ya utendaji duni na kuwa taasisi yenye ufanisi katika utoaji huduma za usafirishaji wa reli nchini.
Aidha mkutano wa Baraza Kuu unatarajiwa kutoa maazimio ya kuboresha maslahi ya Wanareli kwa ujumla na kuimarisha utendaji kazi kwa moyo wa kizalendo, uadilifu na kujituma zaidi.
Maandalizi ya kuziunganisha TRL na Rahco kumefanya mkutano kufanyika katika mazingira ya utulivu na matumaini makubwa. Mkutano umejadi pamoja na mambo mengine taarifa ya kazi ya udhibiti wa mafuriko kati ya maeneo ya stesheni za Gulwe, Kidete na Kilosa.
li trl-bkw-3 trl-bkw-5trl-bkw-4   trl-bkw-8  trl-bkw7trl-bwk-2   trl-bkw-9
1 2 3